Sunday, March 25, 2012

SIMBA YASHINDA BAO 2 - 0 DHIDI YA ES SATIF UWANJA WA TAIFA LEO

 Ubao wa Matangazo ukionyesha matokeo ya mchezo wa leo
  Kikosi cha Simba.
 Kikosi cha Es Satif
 Marefarii na Manahodha wa timu zote mbili.
 Mkono wa kheri kabla ya mtanange kuanza.
 Mshambuliaji wa Timu ya Simba,Salum Machaku (kulia) akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0.
 Mshambuliaji wa Simba,Emmanuel Okwi (kulia) akimtoka beki wa timu ya Es Satif ya nchini Argeria,Farouk Belkaid katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho uliomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0,mabao yaliyopatikana kipindi cha pili cha mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi na Haruna Moshi.
 Ameir Maftah wa timu ya Simba (kulia) akiachia shuti kali kuelekea langoni mwa timu ya Es Satif.
 Beki wa Es Satif (alielala chini) akiondosha hatari langoni mwake wakati Salum Machaku akitaka kujaribu kufunga goli.
 Holaaaaaa..........
 Hatari langoni mwa Es Satif.
 Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Fredrick Sumaye (mwenye suti),Waziri wa Afrika Mashariki,Mh. Samuel Sitta (kulia),Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe pamoja na Mbunge wa Tabora Mjini,Mh. Aden Rage wapo uwanjani hapa kuisapoti timu ya Simba.
 Kocha wa Timu ya Shimba,Milovan Cirkovic (kushoto) akipeana mkono na Kocha wa timu ya Es Satif,Alain Geiger mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho,uliochezwa leo kwenye uwanja wa Taifa jijinin Dar es Salaam.Simba imeshinda bao 2 - 0.
Mashabiki wa timu zote mbili wanavyoonekana.
Mashabiki wa Es Satif wakiwa na huzuni iliyopitiliza.
Onyo kali uwanjani.
 Mashabiki wa Simba wakiwa wamefurika uwanjani hapa.

1 comments:

TFF MNATIA AIBU SANA NA MNAFANYA MPIRA WA MIGUU USIENDELEE TANZANIA, YAANI MCHEZAJI MWASIKA AMEACHIWA HURU WAKATI KUNA VIGEZO VYOTE VINAVYOONYESHA KUWA ALIMPIGA NGUMI MWAMUZI NA HII HADI KWENYE VIDEO KILA MTU AMEONA, HII KWELI NI HAKI HAPA? JE YULE MWAMUZI ALIEPIGWA NGUMI ATAJISIKIAJE NA KAMA AKIWA AMEPATA MADHARA YOYOTE KUTOKANA NA ILE NGUMI? MNATUTIA AIBU WATANZIA NA HATUWEZI KUWA NA FAHARI NA MPIRA WETU HATA KIDOGO.

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation