Michuano ya Kagame Castle Cup 2011 inaanza kesho kutwa (Juni 25 mwaka huu) ambapo viingilio kwa kituo cha Dar es Salaam vitakuwa VIP A sh. 15,000, VIP B sh.10,000, VIP C sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 5,000, viti vya bluu sh.3,000 na sh. 2,000 kwa viti vya kijani. Kwa siku ambazo timu za Yanga au Simba hazitacheza kiingilio cha chini kitakuwa sh. 1,000.
Kwa kituo cha Morogoro ambapo mechi zitachezwa Uwanja wa Jamhuri kiingilio kitakuwa sh. 5,000 kwa ukwaa kuu na sh. 1,000 mzunguko.
Timu zitakazofungaua pazia la michuano hiyo Juni 25 ni Etincelles v Ocean View,Simba v Vitalo huku siku inayofuata ya Juni 26 itakuwa ni kati ya APR v Port,Yanga v El Merreikh. Mechi zote hizo zitaanza saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Timu ambayo imeshawasili mpaka sasa ni Vitalo wakati Elman ya Somalia, Ocean View ya Zanzibar na El Merreikh zinatarajiwa kuwasili leo kuanzia mchana.
Vilevile mtihani wa utimamu wa viungo (physical fitness test) kwa waamuzi watakaochezesha michuano hiyo utafanyika kesho (Juni 24 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi ni Gebremichael Lulesghed –Eritrea, Dilicho Sherefa- Ethiopia, Sylvester Kirwa-Kenya, Wiish Yabarow –Somalia, Hussein El Fadil –Sudan, Israel Mujuni –Tanzania, Ronnie Kalema –Uganda na Ibada Kombo –Zanzibar.
Waamuzi wasaidizi ni Charles Nizigiyimana –Burundi, Egue Yassen Hassan –Djibouti, Mussie Kinde –Ethiopia, Brasan Mamati –Kenya, Simba Honore –Rwanda,Ahmed Waleed –Sudan, Samwel Mpenzu –Tanzania na Mark Ssonko –Uganda.
0 comments:
Post a Comment