Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ataingoza timu hiyo kwenye mechi ya
kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) itakayochezwa Mei 14 mwaka huu
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 kamili jioni.
Awali Poulsen ambaye pia ni mkufunzi wa makocha alikuwa ameteuliwa na Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuendesha kozi ya makocha nchini Gambia
kuanzia Mei 6- 14 mwaka huu. Kozi hiyo imeahirishwa hadi Septemba mwaka huu.
Kikosi cha wachezaji 19 wa Stars kinaingia kambini kesho (Mei 7 mwaka huu)
hoteli ya Atriums jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayo
inazikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza.
Wachezaji walioitwa na Poulsen kwa ajili ya mechi hiyo ni makipa Shabani Kado
(Mtibwa Sugar), Shaaban Dihile (JKT Ruvu) na Juma Kaseja (Simba). Mabeki
niShadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’
(Yanga), Amir Maftah (Simba), Juma Nyoso (Simba) na Kigi Makasi (Yanga).
Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz
(Azam), Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Azam) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).
Washambuliaji ni Machaku Salum (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngasa (Azam), Mohamed
Banka (Simba), John Bocco (Azam) na Mbwana Samata (Simba).
Wachezaji wanaocheza nje ambao wataanza kuripoti wiki ijayo ni Idrissa Rajab
(Sofapaka, Kenya), Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Abdi Kassim (DT Long
An, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (Vancouver
Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden).
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF
0 comments:
Post a Comment