Mlinda mlango wa timu ya soka ya Mkoa wa Manyara, Ally Mohamed ( jezi zambarau) akijiandaa kuokoa mpira wakati ilitotokea heka heka langoni mwake katika mchezo dhidi ya Mkoa wa Morogoro, Moro Stars , katika mashindano ya Kili Taifa CUP , Kituo cha Morogoro uliofanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa, Moro Stars ilishinda bao 1-0. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro
Monday, May 9, 2011
Kili Taifa Cup: moro stars yainyuka manyara 1-0
-Mchezaji wa timu ya Mkoa wa Morogoro , Moro Stars, Dickson Mbeikya ( kulia) akijaribu kufunga kwa kichwa huku Mlinda mlango wa timu ya soka ya Mkoa wa Manyara, Ally Mohamed ( jezi 18) akijiandaa kuokoa mpira huo katika moja ya heka heka zilizotokea langoni mwake , katika mchezo huo wa mashindano ya Kili Taifa CUP , Kituo cha Morogoro uliofanyika jana uwanja wa Jamhuri wa mji Kasoro Bahari. Moro Stars ilishinda bao 1-0.
Mlinda mlango wa timu ya soka ya Mkoa wa Manyara, Ally Mohamed , akiuweka mpira katika himaya ya mikono yake kufuatia shuti kali ililichongwa na mmoja wa washambuliaji wa timu ya Mkoa wa Morogoro, Moro Stars ( hayupo pichani) huku mabeki wa timu yake akihakikisha usalama wake , waksati wa mashindano ya Kili Taifa CUP , Kituo cha Morogoro uliofanyika jana kwenye uwanja wa Jamhuri wa Mjini hapa, Moro Stars ilishinda bao 1-0
0 comments:
Post a Comment