Sunday, May 15, 2011

Habari Kuhusu Ligi ya Taifa

ANGETILE OSIAH, KATIBU MKUU WA TFF

Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa itaanza Juni 11 mwaka huu katika
vituo vya
Sumbawanga, Kigoma, Singida na Kibaha. Washindi watatu wa kwanza wa
kila kituo watashiriki hatua ya fainali itakayofanyika katika kituo
kitakachotangazwa baadaye.

Kituo hicho cha fainali kitakuwa na makundi matatu ya timu nne nne. Mshindi wa
kila kundi na washindwa bora (best losers) wawili, hivyo kufanya jumla ya timu
tano ndizo zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Kituo cha Sumbawanga kitakuwa na timu za Small Kids (Rukwa), Ilonga FC (Mbeya),
Mlale JKT (Ruvuma), Central Police (Dar 3), Tumbaku SC (Morogoro) na mabingwa wa
Iringa. Kituo cha Kigoma kitakuwa na timu za Shinyanga United (Shinyanga), Geita
Veterans (Mwanza), Polisi SC (Mara), Kasulu United (Kigoma), Rumanyika FC
(Kagera) na mabingwa wa
Tabora.

Singida itakuwa na timu za Polisi SC (Arusha), Babati Mashujaa SC (Manyara),
Lang’ata Bora FC (Kilimanjaro), Samaria FC (Singida) na Majengo FC (Dodoma).
Kituo cha Kibaha ni Cosmopolitan (Dar 1), Mgambo Shooting (Tanga), Mailimoja
United (Pwani), Sifapolitan (Dar 2), Liwale Stars (Lindi) na mabingwa wa
Mtwara.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Mei 15 mwaka huu) imesisita kuwa iwapo mikoa ya Tabora, Iringa na Mtwara itakuwa haijawasilisha majina ya mabingwa wao katika muda uliopangwa ligi hiyo itaendelea bila timu zao kuwemo.

Mwisho wa timu kuthibitisha kushiriki na kulipa ada ya ushiriki ya sh. 70,000 ni
Mei 20 mwaka huu. Mei 28 mwaka huu ndiyo siku ya mwisho ya kurudisha fomu za
usajili.

Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation