Thursday, March 24, 2011

Vijana U-23 wakabidhiwa bendera, waelekea Cameroun

MKURUGENZI wa michezo nchini Leonard Thadeo amekabidhi bendera kwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 ambayo imeondoka kuelekea nchini Cameroon kwa mchezo wake wa kwanza utakao chezwa siku ya jumapili.

Timu hiyo ya Ngorongoro Heroes ilicheza mechi tatu za kirafiki mchezo wa kwanza walicheza na Azam FC na kutoka sare ya kwa bao 1-1, kucheza na Mtibwa Sugar na kuifunga kwa bao 1-0 juzi walicheza na Simba na kutoka sare ya bao 1-1 kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo .

Akizungumza wakati akiiaga timu hiyo Thadeo alisema “matumaini ya watanzania wengi ni ushindi kwenye timu hiyo iliiweze kushiriki michuano ya Olimpiki kwa mara ya kwanza na pia nidhamu nikitu muhimu sana ambacho kitaweza kuwasaidia kupata ushindi.

“Nawaomba mfuate yale yote mliofundishwa na makocha na natumaini maandalizi yalikuwa mazuri kwa siku zote mlizokuwa kambini hivyo ushindi ni lazima katika timu yetu."alisema

Naye kocha mkuu wa timu ya vijana wenye umri chinin ya miaka 23 Jamuhuri Khiwelu alisema “timu ipo kamili na inaenda kwenye mashindano, kama mnavyojua kuna kushinda na kushindwa hiyo yote yatakuwa matokeo”alisema Julio

Wakati huohuo naodha wa timu hiyo Salum Terela alisema wanaamini watafuata waliofundishwa na walimu wao na watanzania wawaombee iliwaweze kushinda katika mechi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation