Madaraka Selemani 'Mzee wa Kiminyio' akiongea kwa niaba ya wachezaji wa Simba wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za TFF uwanja wa Karume jijini Dar es salaam mchana huu. Miamba hawa watapambana Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika mchezo wa hisani kuchangia waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
Afisa habari wa Simba SC Clifford Ndimbo akitangaza kikosi cha veterani wa Msimbazi
Afisa habari wa Yanga FC Loius Sendeu akitangaza kikosi cha veterani wa Jangwani
Mratibu wa mpambano huo Suleiman Mathew akifafanua jambo
Mwanahabari Eddo Kumwembe akiwapatanisha wasemaje wa Yanga Loius Sendeu (shoto) na Clifford Ndimbo wa Simba walipotaka kuzichapa kavu kavu kufuatia ubishi wa nani ataibuka kidedea Jumamosi
Kamati ya maandalizi. Kati ni Mwenyekiti Geoffrey shoto in Katibu Moses Mkandawire na kulia ni Makamu Mwenyekiti Ali Martin Maliva
Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura (kulia) akiwa na waandaazi na maofisa habari wa Yanga na Simba mara baada ya mkutano na waandishi wa habari mchana huu
0 comments:
Post a Comment