MFANYABIASHARA Kassim Ally (28), mkazi wa Kichangani jijini Dar es Salaam amepandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke akikabiliwa na tuhuma za kukamatwa na tiketi 74 za viingilio vya mchezo baina ya Yanga na Simba.
Ally alikamatwa kabla ya mchezo huo wa watani wa jadi, Simba na Yanga uliochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kiinglio cha chini kilikuwa Sh 3,500.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu Emmanuel Mbona, Inspekta wa Polisi, Kato Ishengoma alidai kuwa Machi 5 saa 9:00 alasiri mshtakiwa huyo alikamatwa na askari wa doria mwenye namba E 5018 Koplo Mohamed akiwa na tiketi hizo, kinyume cha sheria.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kuwa tiketi hizo mshtakiwa huyo alikuwa akiziuza kwa Sh 4,500 badala ya Sh3,000 ambacho kilikuwa ni kiingilio kilichowekwa na wahusika (TFF).
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21 mwaka huu, itakapotajwa tena.
Chanzo: Mwananchi

0 comments:
Post a Comment