MKURUGENZI wa Michezo nchini Leonard Thadeo amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca Cola ambayo ndiyo wadhamini wakuu wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 (Copa Coca Cola) kuandaa mikakati ya kuhakikisha inalinda vipaji vya wachezaji wote wanaopatika katika michuano hiyo.
Hayo alisema jana katika uzinduzi wa mashindano ya tano ya Copa Coca Cola uliofanyika kwenye ukumbi wa hosteli za TFF jijini.
Akizungumza katika hafla hiyo Thadeo alisema TFF kwa kushirikiana na Coca Cola wanatakiwa kuandaa mikakati ya kuhakikisha wachezaji wote wanapatika katika mashindano hayo wanaendelezwa na siyo kuwaacha wakapotea.
"Nawapongeza Coca Cola kwa kudhamini mashindano haya ya vijana wenye miaka chini ya 17 ambayo lengo lake ni kuibua vipaji vya wachezaji, lakini wasihishie hapo tu wana changamoto kubwa ya kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kuwendeleza vijana wote wanaopatika katika michuano hiyo kwa kushirikiana na TFF pamoja na wadau wengine wa michezo.
"Wanaweza kuanzisha hata kituo cha soka ambacho vijana wote watakaokuwa wakipatika kwenye michuano hiyo ya Copa Coca Cola wanaendelezwa na siyo kuwaacha vipaji vyao vikapotea," alisema Thadeo.
Katika hatua nyingine Meneja wa Coca Cola, Alpha Joseph alisema kuwa kampuni hiyo safari hii inatarajia kutumia zaidi ya Tsh 420 katika udhamini wake wote wa michuano hiyo ambayo tayari imeshaanza kutimua vumbi katika ngazi ya wilaya.
Hatahivyo Kampuni hiyo jana imekabidhi TFF mpira 720, bips 40 kwa kila Wilaya, shilingi 200,000 kwa kila Wilaya kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo kwa ngazi ya Wilaya

0 comments:
Post a Comment