Tuesday, March 8, 2011

TFF yamuombea ruhusu Thomas Ulimwengu TP Mazembe, Mchujo wa timu ya Taifa ya Vijana kufanyika wiki ijayo

SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limeiandikia barua klabu ya TP Mazembe likiomba ruhusa ya kumtumia mshambuliaji Thomas Ulimwengu wakati timu ya taifa ya umri chini ya miaka 23 itakapocheza mechi dhidi ya Cameroon Machi 27.

Hatua hiyo inafuatia Ulimwengu kutakiwa na klabu hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam jana Msemaji wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa ni matumaini ya shirikisho hilo kuwa TP Mazembe litamruhusu mashambuliaji huyo kwa kutambua umuhimu wa kuitumikia timu ya taifa.

"Kimsingi klabu ya TP Mazembe imemtaka Ulimwengu kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio kule na sisi kama TFF tumebariki hilo ambapo anatarajia kuondoka nchini Machi 11.

"Isipokuwa tumewaandikia barua kuwaomba akiwaandaendelea na majaribio yake wamruhusu akaitumikie timu ya taifa ya umri chini ya miaka 23 itakayokuwa inacheza na Cameroon Machi 27 kule Yaunde,"alisema Wambura.'

Ulimwengu ambaye kwa sasa ameweka kambi na kikosi cha timu hiyo kwenye Hoteli ya Bamba Beach pia yupo katika kituo cha soka cha ABC Academy cha Sweden.

Ikiwa Ulimwengu atafanikiwa majaribio hayo katika klabu ya TP Mazembe, hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa kwake na taifa kwa ujumla ukizingatia klabu hiyo ni kubwa na maarufu barani Afrika na Duniani.

Wakati huo huo Wambura alisema kuwa mchujo wa timu hiyo ya vijana ambayo ipo kambini Bamba Beach Kigamboni utafanyika ijumaa ijayo.

Alisema wachezaji watakaopita kwenye mchujo huo watacheza na timu ya vijana ya Uganda Machi 19 au 20.

Wambura alisema kuwa iwapo Uganda itachomoa kucheza na Tanzania timu hiyo ya vijana itajipima na timu moja wapo kati ya Simba, Yanga au Azam Fc kabla ya mechi yao na Cameroon.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation