Sunday, March 27, 2011

TAIFA STARS KIDEDEA DHIDI YA AFRIKA YA KATI, YASHINDA 2-1

Kikosi cha Taifa Stars kilichoibanjua Afrika ya Kati
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Afrika ya Kati, Accorsi Jules (kushoto) akisalimia na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jan Poulsen mara baada ya mchezo wa kuwania kufuvu fainali za mataifa ya Afrika (CAN) kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji wa Taifa Stars, Mohamed Banka akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa timu ya Afrika ya Kati, Manga David (kushoto) na Enza Manasse (12).
Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa
akimtoka beki wa timu ya Afrika ya kati, Manga David.

Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza mshambuliaji wa timu hiyo Mbwana Samata baada ya kuifungia timu yake bao la pili dhidi ya Afrika ya Kati katika mchezo wa kuwania kufuvu fainali za mataifa ya Afrika (CAN) uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana
Mashabiki wa soka wakishangilia ushindi wa Taifa
Stars baada ya kuifunga Afrika ya Kati
.


Taifa Stars imeifunga kishujaa timu ya taifa ya Afrika ya Kati bao 2-1 katika mechi ya awali kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na maelfu ya wapenzi wa soka.

Mechi hiyo ya vuta nikuvute ambayo Stars iliahitaji ushindi ili kujiweka sawa katika mbio hizo za kuwania fainali hizo zitakazofanyika Gabon na Equatorial Guinea, ilishuhudia wenyeji wakipigwa bao mo9ja katika kipindi cha kwanza.

Stars ilisawazisha dakika ya 49 Shaaban Nditi wakati bao la ushindi liliwekwa kimiani na Mbwana Samatta dakika ya 89.

Stars ilicheza mechi ya kwanza na Algeria na kutoka sare ya bao 1-1 kabla ya kufungwa bao 1-0 na Morocco nyumbani.

Ushindi wa mechi ya leo umerejesha imani ya Tanzania kusonga mbele.

Taswira zinakuja baadaye kidoooogo....

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation