Tuesday, March 15, 2011

Poulsen atangaza kikosi cha Taifa Stars cha kuivaa Afrika ya Kati

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa Jan Poulsen, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) wakati wa kutangaza kikosi cha wachezaji wataocheza na timu ya Afrika ya Kati, katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2012, zitakazofanyika Ikweta ya Guinea na Gabon. Kulia ni Ofisa Habari wa Shirkisho hilo, Boniface Wambura.

KOCHA wa timu ya taifa,Taifa Stars Jan Poulsen ametangaa kikosi cha wachezaji 23 kitakachojiandaa kwa mchezo dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuwaita kwa mara ya kwanza kiungo wa JKT Ruvu Mwinyi Kazimoto na mlinda mlango Shaaban Dihile.

Kocha huyo raia wa Denmark Jan Poulsen pia amewatema Jerry Tegete (Yanga), Mohamed Ally 'Shiboli', Kelvin Yondani (Simba), Salum Machaku (Mtibwa) na Said Mohamed kutoka Majimaji wote walikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Cecafa na pia walicheza michuano ya Mto Nile nchini Misri hivi karibuni.

Hata hivyoKazimato na Dihile waliwahi kuichezea Taifa Stars ilipokuwa ikinolewa na Marcio Maximo lakini baadaye aliwatema hadi Poulsen alipotangaza kuwajumuhisha katika kikosi chake alichokitangaza jana Mchezo baina ya Taifa Stars na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao ni wa
kuwania kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika umepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam Machi 26.

Kikosi kamili kilichotangazwa jana mbele wa Wanahabari ni ni pamoja na walinda milango Shaaban Kado, Juma Kaseja na Shaaban Dihile wakati mabeki ni Shadrack Nsajingwa, Aggrey Morris, Nadir Haroub'Canavaro', Stephano Mwasika,Haruna Shamte, Juma Nyoso, na Idrisa Rashid.

Viungo ni Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Jabir Aziz, Henry Joseph, Abdi Kassim na Mwinyi Kazimoto huku washambuliaji ni Dan Mrwanda, Nizar Khalfan, Mrisho Ngasa, Mohamed Banka, Athumam Machupa, John Boko na Mbwana Samata.

Poulsen alitetea uamuzi wake wa kuwaita baadhi ya wakongwe akiwemo Athuman Machupa na Dan Mrwanda kwa kusema uzoefu wao una umuhimu katika kujenga ari ya kikosi kwakua wanajua nini wanachokifanya.

Akizungumzia mchezo huo kwa ujumla Poulsen alisema ni dhairi utakuwa mgumu ukizingatia uzuri wa wapinzani wao ambao waliichapa Algeria Ugenini.

"Tunahitaji pointi nne ili tujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu,tunafahamu wazi kwamba Jamhuri ya Kati si timu rahisi waliifunga Algeria kwao lakini nasisi tunatapa ushindi pia hivyo tutahakikisha tunashinda mechi hiyo,"alisema poulsen.

Alipoulizwa ni vipi amemchagua Kado na Samata katika kikosi chake ili hali anajua wazi wachezaji hao pia wamo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini chini ya miaka 23, Ngorongoro Heroes, Poulsen alisema kuwa zote ni muhimu lakini duniani kote timu ya taifa ya wakubwa ni muhimu zaidi.

Wakati huo huo kocha wa JKT Charles Kilinda alisema kuwa amefurahishwa na uteuzi wa wachezaji wake wawili Dihile na Kazimoto na akamtaka poulsen kuongeza idadi kwani kikosi chake kina wachezaji mahiri wengi.

"Nimefurahi, kwanza nasema alikuwa hatutendei haki alichelewa sana kuwaita lakini pia Poulsen aangalie uwezekano wa kuongeza wengine kwani nina wachezaji wengi mahiri,"alisema Kilinda.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation