KOCHA wa timu ya taifa, Taifa Stars Jan Poulsen amesema kikosi chake kipo tayari kupambana na kuishinda Jamhuri ya Afrika ya Kati kesho kwenye Uwanja wa Taifa hata kama atawakosa nyota wake watatu wanaocheza soka nje ya nchi akiwemo Dan Mrwanda, Abdi Kassim na Nizar Khalfan.
Mrwanda na Kassim wanaocheza soka ya kulipwa nchini Vietnam pamoja na Nizar Khalfan anayesakata kabumbu nchini Canada mpaka sasa hawajajiunga katika kambi ya Taifa Stars licha ya Poulsen kuwajumuisha katika kikosi kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Afrika ya Kati.
Lakini jana kupitia mkutano na Waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)Angetile Osiah alisema kuwa uwezekano wa wachezaji hao kuwepo katika kikosi cha Taifa Stars katika mechi ya kesho ni hafifu kufuatia taarifa za kuwaombea kuruhusa walizotuma kwa klabu zao kutofika hadi wakati huo.
"Tunashanga hatujui kimetokea nini kwa kina Mrwanda, Kassim na Nizar kwasababu barua za kuwaombea ruhusa katika klabu zao hazijafika hadi sasa wakati njia iliyotumika kuwatumia tiketi ni hiyo hiyo, hivyo tunatakiwa kuwaamini wachezaji waliopo kwani huwezekano wa kuwapata tena haupo,"alisema Oseah.
Akizungumzia suala hilo Poulsen alisema:"Taifa Stars ni jeshi lenye wapiganaji wengi na walio tayari kwa mapambano ikiwa wachezaji hao hawatakuwepo basi waliopo watapigana kuhakikisha tunashinda.
"Hii ni vita,kila mmoja anatakiwa kupigana ili ashinde, kifupi tumejiandaa kikamilifu na hatuwadharau wapinzani wetu hata kidogo,"alisema Pouslen.
Naye nahodha wa Taifa Stars Shadrack Nsajigwa alisema kuwa wamejiandaa vya kutosha na wao kama wachezaji watajituma kuhakikisha wanapata matokeo mazuri yatakayowapeleka mbele.
Kwa upande wake kocha wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Jules Acorsi alisema kuwa kama walivyocheza dhidi ya Algeria na Morocco ndivyo watakavyofanya watakavyoikabili Taifa Stars.
"Siijui Tanzania lakini kama tulivyocheza dhidi ya Algeria na Morocco na hivyo hivyo tutacheza dhidi ya Tanzania.
"Nafikiri tunaweza kuwanya kitu ndio maanda utaona hata sasa tunaongoza kundi,"alise,a Acorsi.
Taifa Stars ilianza kampeni yake ya kuwania kufuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa kutoka sare ya bao 1-1 na Algeria ugenini na baada ya hapo ikakutana na kipigo cha bao 1-0 kutoka Morocco.

0 comments:
Post a Comment