Wednesday, March 2, 2011

mstakabali wa Yanga na Simba Jumamosi

Mechi namba 108 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Yanga na Simba itachezwa Jumamosi (Machi 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni kama ifuatavyo;

Viti vya kijani mzunguko ambavyo viko 19,648 ni sh. 3,000

Viti vya bluu mzunguko (17,045) ni sh. 5,000

Viti vya rangi ya chungwa (11,897) ni sh. 7,000

VIP C yenye viti 4,060 ni sh. 10,000

VIP B yenye viti 4,160 ni sh. 20,000

VIP A yenye viti 748 ni sh. 30,000

Tiketi zitaanza kuuzwa Ijumaa saa 2 asubuhi katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Big Bon Msimbazi (Kariakoo), Mgahawa wa Steers uliko Mtaa wa Samora/Ohio na Uwanja wa Uhuru.

Pia siku ya mchezo tiketi zitaendelea kuuzwa katika maeneo hayo kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 6 mchana. Baada ya muda huo zitaendelea kuuzwa Uwanja wa Uhuru pekee.

Mwamuzi atakuwa Oden Mbaga wa Dar es Salaam akisaidiwa na Mohamed Mkono (Tanga) na Maxmillian Nkongolo wa Rukwa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation