Tuesday, March 15, 2011

Mchezo wa Yanga na Ruvu Stars waingiza milioni 19.4

KIASI cha Sh,milioni 19,475,000 kimepatikana kupitia viingilio vya mpambano wa ligi kuu baina ya Yanga na JKT Ruvu uliofanyika Machi 12 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Boniface Wambura alisamesema leo kuwa mapato hayo yalipatikana baada ya watazamaji 4,028 kuingia uwanjani kwa viingilio vya kati ya Sh15,000, sh. 8,000, sh. 5,000 na sh. 3,000.

Wambura alisema kuwa baada ya kulipa asilimia 18 kwa Serikali ambayo ni sh. 2,970,763 ikiwa ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na gharama za awali za mchezo sh. 3,639,600 fedha zilizobaki kwa ajili ya mgawanyo ni sh. 12,864,637.

Alisema katika mgawanyo huo kila timu ilipata mgawo wa sh. 3,859,391, gharama ya Sh. 1,286,464,TFF Sh. 1,286,464, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF Sh. 643,232), Uwanja Sh. 1,286,464, Baraza la Michezo la Taifa BMT Sh. 128,646 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam DRFA Sh. 514,585.

Aidha Wambura alisema mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar iliyochezwa Machi 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru iliingiza kiasi cha Sh Milioni 3,718,000 baada ya kuingiza watazamaji 1,021 waliolipa viingilio vya kati ya Sh,5,000, 3,000 na 2,000.

Wambura alisema baada ya kuondoa gharama za awali za mechi kila timu ilipata Sh, 468,494, gharama ya mchezo Sh,156,165,TFF Sh, 156,165, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu- FDF Sh, 78,082), Uwanja Sh. 156,165,DRFA Sh. 62,466 na BMT sh. 15,616.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation