Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limekiandikia barua Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kiteue kocha msaidizi wa timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 23 (U23) inayojiandaa kwa mechi ya mchujo ya michuano ya Olimpiki dhidi ya Cameroon itakayochezwa Machi 26 mwaka huu jijini Yaounde.
Kocha atakayeteuliwa na ZFA vilevile anatakiwa kuteua wachezaji wasiopungua 10 (kumi) na wasiozidi 15 (kumi na tano) ambao watajiunga na kikosi cha awali cha wachezaji 25 kilichotangazwa juzi na Kocha Mkuu wa timu hiyo Jamhuri Kihwelo.
Baada ya wachezaji hao kutoka Zanzibar kuungana na wenzao kwa ajili ya mazoezi, benchi la ufundi baadaye litafanya mchujo ili kubaki na kikosi cha mwisho cha wachezaji 25 ambacho ndicho kitakachoikabili Cameroon katika mechi ya kwanza na ya marudiano itakayochezwa jijini Dar es Salaam.
U23 inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki. Mechi hizo zitachezwa kati ya Machi 12 au 13 na 19 au 20 mwaka huu. Safari ya Yaounde kwa timu hiyo inatarajiwa kufanyika Machi 22 mwaka huu.
Imetolewa leo na
Boniface Wambura
Ofisa wa Habari, TFF
0 comments:
Post a Comment