Thursday, February 24, 2011

Julio atangaza kikosi cha U-23

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Vijana ya U-23 Jamhuri Kihwelo 'Julio' (kulia) akiwa na Afisa Habari wa TFF Michael Wambura siku walipotangaza kikosi cha timu hiyo jijini Dar es salaam

Kocha mkuu wa timu ya taifa vijana chini ya umri wa miaka 23 JAMHURI KHWELO (JULIO) ametangaza kikosi cha wa chezaji 25 wa kikosi hicho tayari kuikabili CAMEROON katika mchezo wa kuwani kufunzu kwa mashindano ya OLYMPIC jijini LONDON mwakani,mchezo huo wa awali utapigwa mjini YAOUNDE machi 26.

Akitangaza majina ya wachezaji wa kikosi hicho jijini DSM KHWELU amesema wachezaji wa kikosi hicho wamechanguliwa baada ya kuonyesha viwango vya hali ya juu katika mashindano mbalimbali yakiwemo yale ya timu za vijana chini ya umri wa miaka 20 za vilabu vya ligi kuu na fainali ya ligi daraja la kwanza yaliyomalizika jana jijini TANGA.

Kwa upande wake Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF BONIFANCE WABURA amesema shirikisho lake linafanya kila jitihada kuhakikisha timu hiyo ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 inacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa ya kujipima nguvu kati ya MACHI 12 na 13 ama 19 na 20 kabla ya kuivaa timu ngumu ya CAMEROON.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
The Official Blog of Tanzania Football Federation